Tume ya kutetea haki za kibinadamu KHRC inatazamiwa kuandaa hafla ya kumkumbuka wakili wa maswala ya kikatiba marehemu Nzamba Kitonga leo Alhamisi.
Aliyekuwa jaji mkuu Dkt. Willy Mutunga pamoja na mrithi wake David Maraga wanatazamiwa kuhudhuria hafla hiyo jijini Nairobi.
Hafla hiyo itatumika kukumbuka mchango wake katika maswala ya kikatiba na pia juhudi zake katika kuhakikisha kuwa sheria imefuatwa kikamilifu.
Kitonga alifariki dunia Octoba 24 mwaka jana akiwa na umri wa miaka 64 na atakumbukwa pakubwa katika mchango wake wa kuandika katiba ya mwaka 2010.