Wagonjwa 6 zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa wa corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maafa nchini kuwa 1,807.

Katika taarifa waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema kuwa watu 283 wamepatikana na ugonjwa huo na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 103,615.

Idadi ya waliopona imeongezeka na kufika 85,457 baada ya wagonjwa 66 kupona kutokana na ugonjwa huo.

Watu 277 wamelazwa katika hospitali mbalimbali  42 wakiwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi 18 wakisaidiwa na mashine kupumua.

Nairobi inaongoza na visa 196, Busia 16, Kiambu 14, Mombasa 11, Nakuru 8, Uasin Gishu 6, Kajiado na Machakos 5, Kilifi na Kisumu 4.