Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko atashtakiwa kwa ugaidi pindi atakapopona na kuruhusiwa kuondoka hospitalini.

Uamuzi huu umetolewa na hakimu mkuu wa mahakama ya Kahawa West ambaye ameagiza Sonko abaki hospitalini mpaka hali yake iimarike.

Hakimu huyo vile vile amewazuia maafisa wa kitengo cha kupambana na ugaidi ATPU dhidi ya kumhoji Sonko akiwa angali mgonjwa.

Kesi hiyo imehairishwa hadi Febrauri 26 huku Sonko akisalia hospitalini chini ya ulinzi mkali.