Kenya imerekodi visa vipya 147 vya ugonjwa wa corona baada ya kupima sampuli 2,063 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Hii inafikisha 103,014 idadi ya visa hivyo nchini huku waliopona ikifikia 85,250 baada ya kupona kwa watu wengine 242.

Hakuna maafa yoyote yaliyoripotiwa katika muda huo na hivyo idadi ya waliokufa inasalia kuwa 1,795.

Wagonjwa walio katika chumba cha watu mahututi ICU ni 34, 15 wakisaidiwa na mashine kupumua.

Msambao wa visa hivyo ni kama ifwatavyo; Nairobi 107, Kiambu 9, Mombasa 4, Uasin Gishu 4, Laikipia 3, Kajiado 3, Meru 3, Machakos 2, Makueni 2, Nakuru 2, Nyamira, Nyeri, Trans Nzoia, Busia, Embu, Isiolo, Kitui na Kilifi wameripoti kisa kimoja kila mmoja.