‘’Simeon Nyachae ni mzee aliyejitolea kwa hali na mali kulihudumia taifa la Kenya hadi kifo chake. Daima tutakumbuka mchango wake katika taifa’’.

Ndio matamshi yake rais Uhuru Kenyatta alipowaongoza viongozi wengine wakati wa mazishi ya mzee Nyachae nyumbani kwake Kisii hii leo.

Rais Kenyatta kwenye risala zake amewataka viongozi wengine kuiga mfano wa marehemu katika kuwa na nidhamu wanapolihudumia taifa.

Naibu rais William Ruto, kinara wa chama cha ODM Raila Odinga, aliyekuwa makamu wa rais Kalonzo Musyoka pamoja na kinara wa chama cha Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi ni miongoni mwa viongozi waliohutubu kwenye mazishi hayo wakimtaja marehemu kama mtu mwenye bidii kazini.

Aidha nyachae amesifiwa kwa umrufu wake wa kujiunga kwa sias mwaka 1992 ambapo alihudumu kama mbunge kwa miaka 15 na pia waziri wakati wa utawala wa marais wastaafu Daniel Moi na Mwai Kibaki.

Nyachae alifariki tarehe mosi mwezi huu katika hospitali ya Nairobi akiwa na umri wa miaka 89 baada ya kuugua kwa muda mrefu na amesifiwa sana kutokana na mchango wake wa kusaidia haswa kanisa.

Nyachae amezikwa nyumbani kwake nyumbani kwake Nyosia, eneobunge la Nyaribari Chache kaunti ya Kisii.