Rais Uhuru Kenyatta amemtaka naibu wake William Ruto kujiuzulu iwapo haridhishwi na utendakazi wa serikali.

 Rais Kenyatta amemlinganisha naibu wake na nduma kuwili kwa kuikosoa serikali kwa upande mwingine na kisha kujivunia maendeleo yaliyofanywa na serikali iyo hiyo.

Rais Kenyatta amesema haya alipokagua vituo vya afya katika maeneo ya Uthiru na Kiamaiko katika kaunti ya Nairobi ambapo ameendelea kupigia debe ripoti ya BBI.