Kinara wa chama cha ODM ameelezea matumaini yake kwamba idadi kubwa ya mabunge wa kaunti itapitisha mswada wa BBI licha ya pingamizi kutoka kwa baadhi ya watu.

Odinga amedai kuwa wanaopinga mchakato huo wanajaribu kutumia pesa kuwahonga watu kukataa mswada huo ila amesema ana matumaini kuwa utapita hata kwa kura ya maamuzi.

Akizungumza baada ya kukutana na viongozi wa kaunti ya Kajiado, Odinga ameongeza kuwa watazuru kaunti mbalimbali kuwashawishi viongozi kuunga mkono mchakato huo.

Kauli za Odinga zinajiri siku moja baada ya kaunti ya Siaya kuwa ya kwanza kupitisha mswada huo kwa kauli moja.