Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko ametokwa na machozi mbele ya hakimu wa mahakama ya kupambana na ufisadi Douglas Ogoti wakati wa kesi ya ufisadi dhidi yake.

Sonko ameiambia mahakama hiyo ya Milimani kwamba amelia kwa sababu Polisi wameamua kumtafutia mashtaka zaidi kutokana na misimamo yake ambayo haijawafurahisha watu fulani wenye ushawishi mkubwa.

Gavana huyo aliyebanduliwa ameiomba mahakama hiyo kumpa muda wa siku 14 zaidi kujiandaa kwa kesi ya ufisadi inayogharimu Sh14M inayomuandama.

Wakati uo uo

Wabunge Oscar Sudi wa Kapseret na mwenzake wa Kimilili Didmus Barasa wamemtetea Sonko kutokana na kile wametaja kama kuhangaishwa na serikali.

Wawili hao wanadai kuwa masaibu yanayomuandama Sonko ni kutokana na msimamo wake wa kisiasa.