Bunge la kaunti ya Siaya limekuwa la kwanza kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba BBI.

Wawakilishi wadi wa bunge hilo kwa kauli moja wamepitisha mswada huo baada ya kuandaa vikao vya umma kukusanya maoni ya wananchi Jumanne.

Spika wa bunge hilo la Siaya George Okode anatazamiwa kuwasilisha uamuzi huo kwa bunge kama inavyohitajika kisheria.

Kimsingi, mswada huo unahitaji kupitishwa na mabunge ya kaunti yapatayo 24 kati ya 47 chini ya muda wa siku 90.

Haya yanajiri siku moja baada ya kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kuunga mkono kauli za rais Uhuru Kenyatta kuhusu wawakilishi wadi kupewa mikopo ya Sh2M kununua magari.