Baraza la wazee wa jamii ya Gusii na baadhi ya wabunge kutoka kaunti ya Kisii wamekashifu vikali mtafaruku uliozuka jana kati ya mbunge wa Mugirango Kusini Sylvanus Osoro na mwenzake wa Dagoretti Kaskazini Simba Arati waliopigana kwa mazishi.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza hilo James Mutundura, viongozi hao wamesema purukushani hizo hazikustahili na kwamba zimeshusha hadhi ya jamii hiyo.

Kauli za viongozi hao zinajiri huku katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna akitaka asasi husika kumshika mbunge wa Mugirango Kusini Sylvanus Osoro kwa kusababisha vurugu hizo wakati wa mazishi ya babake naibu gavana wa Kisii Joash Maangi.

Naibu rais William Ruto na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga walikuwepo wakati wabunge hao wawili waliamua kukabiliana kwa makonde.