Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga ameunga mkono matamshi ya rais Uhuru Kenyatta kwamba wawakilishi wadi wana haki ya kupewa mikopo ya kununua magari.

Odinga akizungumza jijini Nairobi alipokutana na maMCAs kutoka maeneo mbalimbali nchini amesema haoni ubaya kwa viongozi hao kupewa mikopo ya Shilingi Milioni mbili kununua magari kwani hata wabunge wanapewa mikopo ya Shilingi Milioni saba kununua magari.

Mkutano huo umeandaliwa kuwashawishi viongozi hao wa mashinani kuunga mkono mswada wa BBI baada ya tume ya uchaguzi IEBC kuidhinisha sahihi zaidi ya milioni moja.

Rais Kenyatta alitoa ahadi hiyo ya mikopo alipokutana na wawakilishi wadi wa kutoka eneo la Mlima Kenya katika Ikulu ya rais ya Sagana ambapo aliwarai kupitisha mswada wa BBI ambao upo kwenye mabunge ya kaunti.