Gavana wa Embu Martin Wambora amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa baraza la magavana (CoG) baada ya kumshinda mwenzake wa Tana River Dhadho Godana.
Wambora anachukua wadhifa huo kutoka kwa mtangulizi wake Wycliffe Oparanya wa Kakamega aliyehudumu kwa mihula miwili.
Gavana wa Kisii James Ongwae amechaguliwa kuwa naibu mwenyekiti wa Wambora wadhifa ambao awali ulikuwa unashikiliwa na Mwangi Wa Iria wa Murang’a.
Aliyekuwa gavana wa Bomet Isaac Isaac Ruto ndiye alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa baraza la magavana, akafuatiwa na Peter Munya aliyekuwa gavana wa Meru wakati huo kabla ya gavana wa Turkana Josphat Nanok kuchukua usukani.