Watu 99 wamepatikana na virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita baada ya kupima sampuli 4,758 na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 100,422.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amethibitisha kuwa watu 66 wamepona virusi hivyo na kufikisha idadi hiyo kuwa 83,757.

Watu wengine wawili wamefariki na kufikisha idadi ya maafa nchini kuwa 1,753.

Wagonjwa 476 wamelazwa katika hospitali tofauti tofauti nchini 28 wako katika vyumba vya wagonjwa mahututi 14 wanasaidiwa na mashine kupumua.

Msambao wa virusi hivi ni kama ifuatavyo: Nairobi 57 , Mombasa 6, Kilifi 6, Kiambu 6, Kajiado 2, Embu 4, Bungoma 3, Machakos 3, Kisumu 2, Migori 2, Kakamega 1, Kitui 1, Laikipia 1, Homa Bay 1, Kericho 1, Meru 1, Siaya 1, Turkana 1.