Waziri wa elimu Profesa George Magoha amewataka walimu wakuu wasikubali uhamisho wa wanafunzi waliofukuzwa shuleni kutokana na ukorofi.

Waziri Magoha amesema serikali inaweka rekodi za wanafunzi watakaohusika na visa vya utovu wa nidhamu na matendo yao yatasalia kuwaandama katika maisha yao.

Marufuku ya Magoha inajiri wakati ambapo visa vya utovu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi vinaendelea kushuhudiwa katika shule mbalimbali ya hivi punde ikiwa ni shule ya upili ya Kituro kaunti ya Baringo ambapo mabweni matatu yamechomwa.