Muungano wa walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri KUPPET unataka kuondolewa kwa shule za mabweni katika juhudi za kukabiliana na utovu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi.

Kupitia kwa mwenyekiti wake Omboko Milemba, KUPPET inahoji kuwa kuondolewa kwa shule hizo kutawapa wazazi muda wa kutosha kukaa na wanao na kuwafunza kuwa na nidhamu.

Milemba vile vile amewahimiza wazazi kuwajibikia jukumu lao la kuwasaidia walimu kupalilia adabu kwa watoto wao wanapokuwa nyumbani.

Kauli hizi zinajiri huku shule kadhaa zikifungwa kutokana na ukorofi wa wanafunzi ambao wameharibu mali ya kuchoma shule.