Watu 6 zaidi wamefariki kutokana na virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maafa kuwa 1,750.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe aidha amedhibitisha kuwa watu 141 wamepatikana na virusi hivyo na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 100,193.

Watu wengine 207 wamepona na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 83,625.

Watu 500 wamelazwa hospitalini na wengine 1,340 wanashughulikiwa nyumbani. Idadi ya wagonjwa walio katika chumba cha watu mahututi ni 25.

Msambao katika kaunti ni Nairobi 87, Kilifi 8, Kwale 7 na Taita Taveta 6.