Tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC) imesema imeidhinisha sahihi 1.14M za kufanyia katiba marekebisho kupitia BBI.

Sahihi hizo ni kati ya 4.2M zilizokuwa zimewasilishwa na kamati iliyoongoza mchakato wa kukusanya sahihi hizo.

Kuidhinishwa kwa sahihi hizo ambazo ni idadi inayohitajika kunamaanisha kwamba mswada wa BBI utatumwa katika mabunge yote ya kaunti ambayo ni arobaini na saba.

Kimsingi, mswada huo unahitajikakuungwa mkono angalau na mabunge ya kaunti yapatayo Ishirini na nne.

Iwapo mabunge hayo yataidhinishwa mswada huo, maspika wa bunge la kitaifa na lile la Senate watafahamishwa kuhusu uamuzi huo kulingana na sehemu ya 147 ya katiba.

Iwapo idadi kubwa ya wabunge watapitisha mswada huo, basi utatumwa kwa rais ambaye atatia sahihi kuidhinisha.

Wakati uo huo

Kinara wa chama ODM Raila Odinga amepigia debe ripoti ya BBI baada ya kukutana na viongozi wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini.

Odinga amesema mbali na mengine, BBI itakuwa na manufaa makubwa kwa vijana kupitia kuanzishwa kwa hazina ya vijana kuwapa mikopo kuanzisha biashara.

Waziri huyo mkuu wa zamani vile vile amemsuta naibu rais William Ruto kwa kuendeleza kile ametaja kama siasa za ubaguzi.