Kanisa moja zaidi limechomwa katika eneo la Otamba, Nyaribari chache kaunti ya Kisii na kufikisha idadi ya makanisa yaliyochomwa hadi kufikia sasa kuwa tano chini ya siku saba na mali kuibwa.

Usiku wa kuamkia jana Jumapili, kanisa la Pentecostal liliteketezwa moto na watu wasiojulikana na kuwalazimu waumini kufanya ibada yao chini ya miti.

Baadhi ya nyumba za watu binafsi pia zimechomwa, hali ambayo imewatia wenyeji na hofu.

Wakaazi wanasema huenda msimamo mkali wa kanisa dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo bangi ndio imesbabisha uhuni huo.