Baada ya kukaa nyumbani kwa miezi kadha, sasa ni afueni kwa watoto walio  chini ya umri wa miaka sita baada ya baraza la kidini kuwaruhusu kuanza kuhudhuria ibada.

Mwenyekiti wa baraza hilo lililotwikwa jukumu la kuweka mwongozo wa ufunguzi wa maabadi, kasisi Anthony Muheria anasema makanisa sawia na misikiti saa inaweza kurejelea vipindi vya watoto ikiwemo Sunday School, Sabbath School na Madrassa.

Baraza hilo limesema limechukua hatua hiyo kutokana na kuendelea kupungua kwa maambukzii ya virusi vya corona.