Baraza la Magavana (CoG) limemhongera Anne Kananu Mwenda kufuatia uteuzi wake kuwa naibu gavana wa Nairobi.

Baraza hilo kupitia mwenyekiti wake Wycliffe Oparanya limesema Kananu ataleta uzoefu wake wa muda mrefu katika uongozi wa jiji la Nairobi baada ya kuongoza kitengo kinachosimamia mikasa katika serikali za kaunti.

Oparanya aidha amelitaka shirika la NMS sawa na wakaazi wa Nairobi kumuunga mkono kikamilifu ili kumuwezesha kufanikisha ajenda ya kuleta maendeleo jijini.

Baraza hilo vile vile limeahidi kumuunga mkono Kananu anapowajibikia majukumu yake ya kuwahudumia wana Nairobi.

Kananu ni naibu gavana wa Nairobi baada kupokezwa mikoba na spika Benson Mutura ila mahakama imetoa agizo linalomzuia kuapishwa kama gavana hadi kesi iliyowasilishwa itakaposikilizwa.