Madaktari wa kaunti ya Mombasa ambao wamekuwa wakigoma wamesitisha mgomo huo baada ya kutia saini maelewano ya kurejea kazini na serikali ya gavana Hassan Joho.

Katibu mkuu wa muungano wa madaktari KMPDU eneo la Pwani Abidan Mwachi anasema miongoni mwa makubaliano yaliyoafikiwa ni kurejeshwa kazini kwa madaktari wapatao 86 waliofutwa kazi.

Miongoni mwa madaktari waliokuwa wamepigwa kalamu ni kaimu katibu mkuu wa muungano wa madaktari nchini KMDPU Dkt. Chibanzi Mwachonda.