Mwanaume aliyekiri kuwabaka na kuwapachika mimba binti zake wawili katika eneobunge la Ndia kaunti ya Kirinyaga amehukumiwa kifungo cha miaka mia moja na arobaine gerezani.

Hakimu Mkuu wa mahakama ya Baricho Anthony Mwicigi amemhukumu kifungo cha miaka sabini John Gichira kwa kila kosa la ubakaji alilotekeleza.

Hii ina maana kuwa Gichira ambaye anaripotiwa kuwa mchungaji wa kanisa moja eneo hilo atasalia korokoroni hadi kifo chake kwa kuwabaka bintize wenye umri wa miaka 14, na 16 mtawalia.

Gichira alikiri kuwabaka bintize siku tofauti mwezi Agosti mwaka uliopita katika kijiji cha Kianyakiru eneobunge la Ndia.

Wawili hao wana mimba ya miezi saba na tano mtawalia.