Aliyekuwa mbunge wa Laikipia mashariki Anthony Mutahi Kimaru amekanusha mashtaka ya kuiba cheti cha kumilki ardhi yenye thamani ya shilingi million 18.5.

Akifika mbele ya hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani Martha Mutuku, mbunge huyo wa zamani amekanusha kuwa tarehe tano Agosti mwaka 2016 aliiba cheti cha kumilki kipande cha shamba kilichoko mjini Nanyuki kutoka kwa makao makuu ya afisi za wizara ya ardhi kaunti ya Nairobi.

Kimaru amekabiliwa na kosa lingine la kujaribu kuuza shamba hilo tarehe tatu Agosti mwaka 2009 akifahamu fika kuwa si shamba lake.

Hakimu Mutuku amemuachilia mshukiwa kwa dhamana ya shilingi million moja au laki tatu pesa taslimu.

Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 28 mwezi huu.