Watu 98 wamepatikana na virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 98,432.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema wagonjwa wengine 154 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 81,255, wagonjwa wengine 3 wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi ya walioaga kuwa 1,716.

Wagonjwa 696 wamelazwa hospitalini na wengine 2,116 wakishughulikiwa nyumbani, 32 wako katika chumba cha hali mahututi.

Maambukizi katika kaunti ni kama ifuatavyo; Nairobi 49, Mombasa 14, Uasin Gishu 8, Kiambu 8.