Tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa (NCIC) inaonya kuhusu uwezekano wa kutokea kwa ghasia nchini iwapo mchakato wa BBI hautaendeshwa kwa njia inayostahili.

Kamishna wa tume hiyo Abdulaziz Farah akizungumza mjini Nakuru amewataka wanasiasa kuwa makini na matamshi yao ili kuepuka kuligawanya taifa hili kwa misingi ya kikabila.

Tume hiyo aidha imeelezea wasiwasi wake kuhusu uwezekano wa kufufuliwa kwa makundi haramu ambayo huenda yakatumika kuelekea uchaguzi mkuu wa 2022.