Katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini COTU Francsi Atwoli amemtetea waziri wa elimu Profesa George Magoha kwa kumtusi mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Uasin Gishu Gitonga Mbaka.

Atwoli ambaye ameitaka tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC iache kumchunguza Magoha anasema waziri huyo hakuwa na makosa yoyote na kwamba alikuwa anajaribu kuhakikisha kuwa nidhamu imezingatiwa.

Matamshi hayo ya Magoha yamesababisha hamaki kutoka kwa maafisa wa elimu na kusababisha EACC kuanzisha uchunguzi kwa minajili ya kumuadhibu Magoha.

Tayari Mbaka ameandikisha taarifa na EACC kufuatia tukio hilo lililotajwa na wengi kama lililomshusha hadhi.