Tume ya maadili na kupambana na ufisadi (EACC) imewatahadharisha magavana dhidi ya kujaribu kutafuta njia za mkato kuhepa kushtakiwa kwa ufisadi.

 Afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo Twalib Mbarak katika taarifa amesema pendekezo la baraza la magavana kwa BBI kwamba wasishtakiwe kwa matumizi mabaya ya fedha ni njama ya kukwepa mkono wa sheria na hilo halitakubalika.

Kwa mujibu wa EACC, uchunguzi wao umebaini kuwa baadhi ya magavana wamebuni mbinu za kuhepa lawama wanapoiba pesa za umma ikiwemo kuwapa maelekezo ya mdomo wadogo zao pamoja na kuanzisha kampuni na wendani wao ili kujipa zabuni za kaunti.

Tume hiyo imeonya kuwa iwapo pendekezo hilo litakubaliwa, basi tabia ya watu kuvunja sheria pasipo kujali wala kubali itakita mizizi.