Kwa mara ya kwanza Kenya imeandikisha idadi kubwa ya maafa yanayotokana na ugonjwa wa corona baada ya watu 21 kufariki katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Hii inafikisha 1,072 idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa huo kufikia sasa.

Watu wengine 1,008 wameambukizwa virusi hivyo baada ya kupima sampuli 6,038 na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 59,595.

Vilevile, watu 802 wamepona kutokana ugongwa huo na kufikisha jumla ya watu waliopona kuwa 39,193.

Kwa mujibu ya wizara ya afya, watu 1,262 wamelazwa katika hospitali  mbalimbali, wengine 62 wamelazwa katika chumba cha watu mahututi ICU, 31 wanasaidiwa na mashine kupumua.

Msambao wa visa hivyo ni kama ifuatwavyo: kaunti ya Nairobi inaongoza kwa kunakili visa 417, Mombasa 87, Kiambu 51, Kajiado 48, Nakuru 35, Kisumu & Kakamega 32,Trans Nzoia 26, Kilifi 24, Nyandarua, Kericho, Uasin Gishu 23, Nyamira 21, Machokos 20, Migori 16 na Nyeri 15.