Watu 724 wamepatikana na virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita baada ya sampuli 5,085 kupimwa na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 56,601.

Waziri wa afya Mutahi kagwe anasema idadi ya maafa nchini imefika 1,027 baada ya wagonjwa 14 zaidi kufariki kutokana na ugonjwa huo.

Watu wengine 248 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona nchini kuwa 37,442.

Wagonjwa 54 wako katika vyumba vya watu mahututi (ICU) na wengine 28 wakisaidiwa na mashine kupumua.

Wakati uo huo

Waziri wa afya Mutahi Kagwe kwa mara nyingine amewataka wanasiasa kusitisha mikutano ya kisiasa nchini wakati ambapo visa vya ugonjwa wa corona vinaendelea kupanda.

Badala yake Kagwe ametoa wito kwa viongozi kuweka mbele maisha ya Wakenya kwani kupitia mikutano hiyo ya kisiasa wanahatarisha maisha yao.

INSERT: KAGWE ON WANASIASA

Gavana wa Machakos Dkt. Alfred Mutua anayemezea mate wadhifa wa urais kwenye uchaguzi mkuu wa 2022 amekuwa wa kwanza kutangaza kuwa anahairisha mikutano yake katika maeneo mbalimbali nchini kufuatia kuongezeka kwa visa vya ugonjwa huo.

Yakijiri hayo

Utatozwa faini ya Sh20,000 iwapo utapatikana bila barakao katika maeneo ya umma.

Haya yamedokezwa na Inspekta mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai ambaye hata hivyo amesema maafisa wa Polisi hawataruhusiwa kutumia nguvu wanapotekeleza agizo hili.