Watu 18 zaidi wameaga dunia kutokana na ugonjwa wa corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya waliofariki kuwa 920.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amedhibitisha kuwa watu wengine 220 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 34,429.

Idadi ya maambukizi nchini imeongeza na kuwa 49,997 baada ya watu wengine 276  kupatikana na ugonjwa huo baada ya kupima sampuli 2,126.

Msambao wa visa hivyo ni kama ifuatavyo; Mombasa 71, Machakos 58, Nairobi 50, Kilifi na Busia 21, Kwale 19, Kajiado 13,Garissa 6, Nakuru 5, Narok 4,Makueni na Kiambu 3,Taita Taveta na Tharaka Nithi 1.