Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa chama cha ODM Raila Odiga kwa sasa wanafanya mkutano wa faragha na baadhi ya viongozi kutoka eneo la Nyanza katika mkahawa mmoja kaunti ya Kisumu.

Mkutano huo unatazamiwa kujadili mausla ya maendeleo katika eneo hilo na pia Rais Kenyatta na Odinga wana wanatazamiwa kuwarahi viongozi hao kuunga mkono ripoti ya BBI.

Baada ya mkutano huo, Rais Kenyatta anatazamiwa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika eneo hilo ikiwemo ukarabati wa bandari ya Kisumu, ujenzi wa uwanja wa kimataifa wa michezo wa Jomo Kenyatta eneo la Mamboleo ambao umegharimu shilingi 1.4B

Rais pia anayendamana na upinzani Raila Odinga anatazamiwa kukagua ujenzi wa eneo la kibiashara la Uhuru na pia bustani ya Jaramogi Oginga Odinga inayotazamiwa kutumiwa na wafanyibiashara mbalimbali.

Hiyo jana, Rais Kenyatta alizuru kaunti ya Nyamira baada ya kupokea ripoti ya BBI Katika kaunti jirani ya Kisii ambapo alizindua ujenzi wa barabara ya kilomita 45 ya Chebilat-Ikonge-Chabera-Nyamusi inayogharimu shilingi billion 3.1.