Watu 296 wamepona virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 27,331

Katibu mkuu wa wizara ya afya dkt. Rashid Aman amethibitisha kuwa idadi ya maafa kutokana na ugonjwa huo imefika 743 baada ya watu 8 zaidi kufariki kutokana na ugonjwa huo.

Watu 137 wamepatikana na virusi hivyo na kufikisha idadi ya maambukizi kuwa 39, 586.

Msambao wa visa hivyo ni kama ifwatavyo; Nairobi 64, Turkana 34, Mombasa 12, Kiambu 8, Uasin Gishu 6 na Trans Nzoia 2.