Mbunge wa Nakuru Mashariki David Gikaria amekamatwa kuhusiana na maandamano yaliyoshuhudiwa mjini Nakuru leo.

Wafanyibiashara pamoja na wahudumu wa matatu waliandamana kulalamikia hatua ya kufurushwa katikati mwa jiji na serikali ya kaunti ya Nakuru.

Iliwalazimu maafisa wa Polisi kutumia vitoa machozi kutibua maandamano hayo huku waandamanaji wakimlaumu Gavana Lee Kinyanjui kwa kukosa kuwasaidia.