Rais Uhuru Kenyatta ni miongoni mwa Marais ambao wanatazamiwa kuhudhuria mkutano wa 75 wa baraza kuu la umoja wa mataifa unaongoa nanga leo.

Mkutano huo ambao unaandaliwa jijini New York, Marekani utafanyika kwa njia ya mtandao kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Mkutano huo utajadili janga la corona, mabadiliko ya hali ya anga, umaskini, njaa na ugaiid ni miongoni mwa yale ambayo yatajadiliwa.

Viongozi wa kudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa akiwemo Rais wa Marekani Donald Trump na Xi Jinping wa Uchina watatoa hotuba yao.