Aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya bandari nchini KPA Daniel Manduku na mshtakiwa mwenza wameachiliwa kwa dhamana ya Sh12M baada ya kukanusha mashtaka ya kuhusika na ufujaji wa Sh923M.

 Manduku amefikishwa mbele ya hakimu mkuu wa mahakama za Milimani Lawrence Mugambi ambapo pia ameshtakiwa pamoja na afisa wa kpa Juma Fadhili wote wakikabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwemo kushirikiana kutekeleza uhalifu wa uchumi pamoja na utumizi mbaya wa afisi.

Manduku alijisalimisha kwa maafisa wa EACC kwa kudaiwa kulipa shilingi milioni mia mbili arobaini na nne kwa wanakandarasi kwa kazi ambayo hawakuwa wameimalizia.