Chama cha ODM sasa kinasema taarifa yake ilieleweka visivyo, na kwamba hawatetei washukiwa wa wizi wa mali ya umma.

Katika taarifa, kiongozi wa chama hicho cha Chungwa Raila Odinga anasema msimamo wa chama hicho ni kuwa serikali inafaa kufanya ukaguzi wa kina kubaini iwapo kweli pesa hizo ziliibwa na ni nani alihusika.

Odinga anasema chama chake hakitawasaza hata maafisa wake wakuu, jamaa au hata rafiki zao ambao wamepora mali ya umma na sasa anataka uchungzui wa haraka kufanywa ili wahusika wakamatwe.