Wafanyibiashara wa nguo za mitumba katika kaunti ya Nakuru wameshiriki maandamano asubuhi hii kulalamikia kile wanadai ni kukosa bidhaa za kuuza.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa muungano wa wauza mitumbi eneo hilo Johnson Maina, wafanyibiashara hao wanasema licha ya serikali kuondoa marufuku ya uagizaji wa nguo hizo nchini, hawana ufahamu ni kwa nini hawawezi kupata bidhaa hizo.

Maina anasema huenda serikali inachelewesha kutoa idhini ya uagizaji wa nguo hizo kutokana na hofu ya mamabukizi ya corona.

Wafanyibiashara hao wanalalama kuw kwa sasa wamelazimika kufungua biashara zao ambazo walikuwa wanazitegemea kujikimu kimaisha.