Waziri wa elimu Prof. George Magoha ameagizwa kukutana na mlalamishi aliyewasilisha kesi mahakamani kupinga kufunguliwa kwa shule na kuelewana.
Mahakama imetoa uamuzi huu baada ya mlalamishi Enock Aura kuwasilisha kesi mahakamani kupinga agizo la Magoha kuwataka wanafunzi wa darasa la nne, wale wa darasa la nane na kidato cha nne kufungua shule Jumatatu ijayo.
Jaji J.A Makau vile vile amemuagiza waziri wa elimu kukutana na wadau wote katika sekta ya elimu ili kuafikiana kuhusu swala hilo.
Pande husika zimeagizwa kurejea mahakamani na maelewano kabla ya Octoba 14.
Yakijiri hayo.
Waziri wa elimu Profesa Goerge Magoha amesema serikali tayari imetoa pesa za kufadhili elimu bila malipo na zitafika shuleni kufikia kesho.
Akizungumza mjini Kisumu, Profesa Magoha amesema ameridhishwa na namna shule zimejiandaa kabla ya kufunguliwa tena baada ya kufungwa kufuatia janga la corona.