Kwa mara ya kumi hii leoJumanne alasiri, maseneta wanatazamiwa kujadili mswada tata wa ugavi wa mapato baada ya kushindwa kuafikiana kuhusu mfumo unaofaa kutumika kugawa pesa katika serikali za kaunti.
Bunge hilo lilibuni kamati ya watu kumi na mbili kutanzua utata huo kwa kuafikia suluhu litakalohakikisha kuwa kila kaunti imepata mgao wake pasipo kufinywa.
Itakumbukwa kwamba hali ya sintofahamu inayozingira mswada huo umesababisha kaunti zote kukosa pesa kuendesha shughuli zake ikiwemo kulipa mishahara hali ambayo imewafanya magavana kutishia kuwatuma nyumbani wafanyikazi wake kufikia Septemba 17.