Kesi za ufisadi zitashughulikia kwa muda wa miezi sita pekee iwapo mtanichagua kuwa rais kwenye uchaguzi mkuu wa 2022.
Ndio ahadi anayotoa gavana wa Machakos Dkt. Alfred Mutua akizindua rasmi azma yake ya kumrithi rais Uhuru Kenyatta anapohitimisha muhula wake wa pili.
Kiongozi huyo wa chama cha Maendeleo Chap Chap ameahidi kushughulikia tatizo la ukosefu wa ajira na kupambana na umasikini miongoni mwa Wakenya iwapo atashinda uchaguzi huo.
Gavana huyo aidha ameahidi kulipa taifa hili mwamko mpya kupitia uongozi bora unaozingatia maendeleo.