Baadhi ya wabunge wa chama cha Jubilee wendani wa naibu rais William Ruto sasa wanadai kuwa watu wa karibu wa rais Uhuru Kenyatta wanahusishwa na sakata ya kupotea kwa pesa za corona katika shirika la kununua dawa na vifaa vya matibabu KEMSA.
Wabunge hao Oscar Sudi wa Kapseret na mwenzake wa Kimilili Didmus Barasa wanadai kuwa wendani wa rais wakiongozwa na mwenyekiti wa chama cha Jubilee David Murathe wamehusika na sakata hiyo ilhali bado hawajakamatwa na kushtakiwa.
Wabunge hao aidha wamemkemea waziri wa Mazingira Keriako Tobiko kwa kumdhalalisha naibu rais huku wakimsuta kwa kufeli katika majukumu yake alipokuwa mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma.