Tume ya huduma za mahakama (JSC) imekosoa mfumo utakaotumika kubuni tume ya kupokea malalamishi kuhusu utendakazi wa idara ya mahakama (Ombudsman) kama inavyopendekezwa kwenye mswada wa BBI.
Jaji mkuu David Maraga ambaye ni mwenyekiti wa JSC anasema kumpa rais mamlaka ya kumteua atakayeongoza tume hiyo itatoa mwanya wa kuhitilafiana na uhuru wa idara ya mahakama.
Na iwapo ni sharti tume hiyo ibuniwe, JSC inataka kupewa jukumu la kumteua atakayekuwa kiongozi na wala sio rais.