Watu tisa wamefariki baada ya kuangukiwa na mashine ya ujenzi katika eneo la Kilimani, Nairobi.

OCPD wa Kilimani Andrew Mbogo amesemaa ajali hiyo imetokea wakati wafanyikazi hao walikuwa wanajaribu kuvunja mashine hiyo baada ya kumaliza kazi.

Ujenzi wa jumba la ghorofa kumi na nne ulikuwa unaendelea mkabala na makao makuu ya idara ya ulinzi (DoD).