Wagonjwa 16 zaidi wamefariki kutokana na virusi vya corona na kufikisha idadi ya maafa nchini kuwa 3,124.

Wizara ya afya imedhibitisha visa vipya 344 baada ya kupima sampuli 4,864 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya visa hivyo kuwa 170,041.

Kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo kwa sasa kiko katika asilimia 7.1% huku waliopona wakifikia 116,018 baada ya kupona kwa watu 30 zaidi.

Kufikia sasa, watu 966,433 wapewa chanjo kati yao wakiwa ni wahudumu wa afya 274,791, walimu 165,995 na maafisa wa usalama 81,729.