Kamati ya pamoja ya bunge kuhusu sheria imewasilisha ripoti yake kuhusu  mswada wa BBI wa mwaka 2020 kwa spika wa bunge la seneti Ken Lusaka.

Iwapo au la kutakuwepo na kikao maalum cha maseneta kujadili mswada huo, Lusaka anasema atawasiliana na viongozi wa wengi na wachache katika bunge hilo iwapo kuna haja.

Akimkabidhi ripoti hiyo, mwenyekiti wa kamati ya sheria katika bunge hilo seneta Okongo Omogeni amesema jukumu sasa ni kwa bunge kuidhinisha ripoti hiyo kabla ya kuandaliwa kwa kura ya maamuzi.

Haya yanajiri siku mbili tu baada ya kamati hiyo ya pamoja kukiri kuwepo kwa dosari katika nakala za mswada huo zilizowasilishwa katika baadhi ya kaunti.

Dosari hizo zinatazimiwa kuibua mjadala mkali bungeni wakati wa vikao vya kujadili mswada huo.