Waziri wa barabara katika kaunti ya Narok John Marindany amefariki kutokana na kile kinaripotiwa kuwa matatizo yanayoambatana na virusi vya corona.

Gavana wa Narok Samuel Tunai amedhibitisha kifo cha waziri huyo na kusema ni pigo kubwa kwa serikali yake.

Katika rambirambi zake, Gavana huyo amemtaja mwendazake kama mtu mpole na mchapa kazi ambaye serikali yake ilitegemea kufanikisha ajenda ya maendeleo.

Hata hivyo Gavana Tunai hajadhibitisha iwapo marahemu aliangamizwa na virusi vya corona.