Aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga hakutuma maombi yake kutaka kupeperusha bendera ya urais kupitia kwa chama cha ODM.

Katibu mkuu wa chama hicho Edwin Sifuna amesema taarifa waliyotuma Aprili 1 kwa wanahabari ilikuwa ya utani tu kuadhimisha siku ya wajinga.

Sifuna sasa anasema baada ya kukamilika makata ayaliyowekwa waliotuma maombi yao ni manaibu viongzoi wa chama hicho, magavana Ali Hassan Joho wa Mombasa na Wycliffe Oparanya wa Kakamega.

Sifuna anasema wawili hao watapigwa msasa kabla ya kumenyana kupata atakayepeprusha bendera ya Chungwa katika uchaguzi mkuu ujao.