Gavana wa Kisumu Profesa Peter Anyang Nyongo amewasimamisha kazi maafisa wa kaunti walionaswa kwenye video wakimburuta mama mmoja kwa lami.

 Gavana Nyongo ambaye ameelezea kusikitishwa kwake na kudhulumiwa kwa mama huyo ambaye ni mchuuzi amelaani kitendo hicho na kuagiza uchunguzi wa kubaini kilichojiri.

Meneja wa jiji la Kisumu Abala Wanga amesema maafisa hao watachukuliwa hatua za kinidhamu baada ya kukamilika kwa uchunguzi.

Wanga hata hivyo anasisitiza kuwa mwanamke huyo alishikilia gari hilo likiondoka na kwamba maafisa hao walikuwa wanahofia kushambuliwa na wahduumu wa bodaboda.

Mama huyo aliyetambulika kama Beatrice Magolo amewaambia wanahabari kuwa alizingirwa na maafisa hao ambao walianza kumsukuma ndani ya gari lao, na alipokataa wakamshikilia mikono na kumburuta gari likienda.