Muungano wa mashirika ya sekta ya kibinafsi KEPSA unitaka serikali kurejesha masharti makali ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Katika taarifa, KEPSA inataka kafyu kuanza kutekelezwa kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi asubuhi.

Muungano huo pia unataka Rais Uhuru Kenyatta kutoa amri ya kutotoka wala kuingia katika katika kaunti tano ambazo zimeshuhudia maambukizi ya juu, ikiwemo Nairobi, Kiambu, Mombasa, Nakuru na Kajiado kwa muda wa majuma mawili.

Muungano huo umeelezea kutamasuhwa kwake na kuendelea kuongezeka kwa visa hivyo na kusema hatua hizo ndizo zitasaidia kukabili hali hiyo.