Chama tawala cha Jubilee kimetangaza majina ya wawaniaji wake kwenye chaguzi ndogo za Garissa, Juja na Bonchari.

Katibu mkuu wa chama hicho Raphael Tuju amesema Abdul Yusuf atawania kiti cha useneta kaunti ya Garissa, Susan Waititu atawania kiti cha ubunge Juja na Zebedeo Opore atawania kiti cha ubunge cha Bonchari.

Abdul Yusuf analenga kumrithi babake Yusuf Hajji huku Susan Waititu akitazamia kumrithi mumewe marehemu Francis Wakapee.

Chaguzi hizo ndogo zimeratibiwa kuandaliwa mnamo tarehe 18 mwezi Mei mwaka huu.

Kiti cha Garissa kilisalia wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa seneta Yusuf Haji, wakaazi wa Jujaji wakasalia bila mbunge kufuatia kifo Francis Waititu na kile cha Bonchari kikasalia wazi kufuatia kifo cha mbunge Oroo Oyioko.